TALIBAN WAVAMIA SHULE NA KUUA 100 PAKISTAN

TALIBAN WAVAMIA SHULE NA KUUA 100 PAKISTAN

Like
334
0
Tuesday, 16 December 2014
Global News

TAKRIBAN watu 100 wakiwemo wanafunzi 80 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia shule moja inayosimamiwa na jeshi huko Peshawar kaskazini – magharibi mwa Pakistan.

Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi.

Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni hapo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi . Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi wakati shambulizi hilo lilipotokea .

Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la hatari.

TALL

Wanajeshi wakijiandaa kuwakabili wanamgambo wa Taliban

 

Comments are closed.