TALIBAN YATIMULIWA KUNDUZ

TALIBAN YATIMULIWA KUNDUZ

Like
279
0
Thursday, 01 October 2015
Global News

MAAFISA wa Afghanistan wanasema kuwa wamedhibiti maeneo muhimu ya mji wa kaskazini wa Kunduz kutoka kwa wapiganaji wa Taliban.

Oparesheni iliotekelezwa usiku kucha imesababisha kuchukuliwa kwa maeneo muhimu ya serikali mbali na kusababisha uharibifu mkubwa kwa wapiganaji.

Lakini wapiganaji wa Taliban wanasisitiza kuwa wanashikilia maeneo makubwa ya mji huo.

Comments are closed.