TAMISEMI YAWAFUKUZA KAZI WAKURUGENZI WALIOHARIBU CHAGUZI ZA SERIAKALI ZA MITAA

TAMISEMI YAWAFUKUZA KAZI WAKURUGENZI WALIOHARIBU CHAGUZI ZA SERIAKALI ZA MITAA

Like
333
0
Wednesday, 17 December 2014
Local News

OFISI ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI- imetoa maamuzi ya kutenguwa uteuzi, kuwasimamisha kazi, na kutoa onyo kali kwa wakurugenzi walioshindwa kutekeleza wajibu wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 mwaka huu.

Akitangaza maamuzi hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI- HAWA GHASIA amesema wizara yake imetekeleza wajibu wake kwa kutoa mafunzo na kuwezesha kifedha, hivyo kasoro zilizojitokeza ni uzembe uliofanywa na watendaji hao na hivyo wanapaswa kuwajibishwa.

Mheshimiwa GHASIA amewataja Wakurugenzi ambao uteuzi wao umetenguliwa kuwa ni ABDALLAH NGODA kutoka Kaliuwa, Tabora, MASALU MAYAYA kutoka Kasulu, Kigoma, BENJAMINI MAJOYA kutoka Mkuranga, GOODY PAMBA na JULIUS MADIGA kutoka Serengeti na SIMON MAYEYE kutoka bunda.

Comments are closed.