TAMWA: NDOA ZA UMRI MDOGO NI UBAGUZI WA KIJINSIA

TAMWA: NDOA ZA UMRI MDOGO NI UBAGUZI WA KIJINSIA

Like
280
0
Friday, 13 February 2015
Local News

CHAMA cha wanawake wanahabari Tanzania -TAMWA kimesema ndoa za umri mdogo ni aina ya ubaguzi wa kijinsia ambao unawagusa wasichana wadogo na hivyo kupelekea kukatisha masomo yao.

Akizungumza na EFM kaimu Mkurugenzi wa TAMWA GLADNESS MUNUO amesema kuwa ubaguzi huo unawafanya wawe waathirika kwa kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa urahisi wakilinganishwa na wenzao ambao hawajaolewa.

Amesema kuwa ndoa za umri mdogo ni swala la afya pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu lakini wasichana wengi walioolewa kwa umri mdogo wana uwezekano wa kuathiriwa na fistula na vifo vya kina mama kwa kuwa miili yao bado haijawa na uwezo wa kuhimili hali hiyo.

 

Comments are closed.