CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa TAMWA, utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo.
Takwimu hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga alipokuwa akifungua semina hiyo.