WIZARA ya Nishati na Madini imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi One na Two unakamilika ifikapo mwezi Februari mwaka 2016 na kuanza uzalishaji ili kuongeza kiasi cha nishati ya umeme kufikia zaidi ya Megawati 100.
Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini dokta Medadi Kalemani alipofanya ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo dokta Kalemani amewapongeza watendaji wa TANESCO na wakandarasi wanaosimamia uendeshaji wa mitambo hiyo ya uzalishaji kuongeza jitihada za dhati kwani watanzania bado hawaridhishwi na kiasi cha umeme kinachozalishwa kwa sasa.