IKIWA ni miaka 40 tangu kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya, wito umetolewa kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha inaendeleza ushirikiano na jumuiya ya umoja huo.
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaamu na balozi wa jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya Filiberto Sebregondi wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye kuelezea ushirikiano kwa vitendo baina ya jumuiya ya ulaya na nchi za Afrika Mashariki.
SEGREGONDI ameeleza kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo umedunu kwa muda mrefu kutokana na kuwepo na utekelezwaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo ikwemo kilimo, huduma za jamii na nishati mbadala.