TANZANIA KUPAMBANA NA UHALIBIFU WA TABAKA LA OZONE

TANZANIA KUPAMBANA NA UHALIBIFU WA TABAKA LA OZONE

Like
369
0
Friday, 07 November 2014
Local News

TANZANIA imesema ipo tayari kuendeleza juhudi za kimataifa za kupunguza kuendelea kuliwa kwa tabaka la ozone kwa kuhakikisha kwamba inatunza misitu na kuwaelimisha wananchi juu ya menejimenti ya misitu hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira , Mheshimiwa Binilith Mahenge wakati wa kufungua kikao cha 13 cha wadau wanaotekeleza program ya kutunza misitu ya Umoja wa Mataifa kinachofanyika Ngurdoto mjini Arusha.

Amesema ingawa Tanzania kwa sasa ina hekta milioni 48.1 za misitu na mapori ambayo sawa na asilimia 55 ya eneo lake, Tanzania kupitia misitu hiyo inanyonya zaidi ya tani milioni 76 za hewa ya ukaa ingawa yenyewe inatoa chini ya tani hizo.

 

Comments are closed.