TANZANIA KUUKABILI UMASIKINI VIJIJINI

TANZANIA KUUKABILI UMASIKINI VIJIJINI

Like
244
0
Thursday, 23 October 2014
Local News

WAKATI Taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inaonyesha ongezeko la watu wanaoishi katika umaskini  Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Tanzania imetaka utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya mwaka 2015 ujielekeze katika kuukabili Umasikini wa Vijijini.

Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi TUVAKO MANONGI, ameeleza hayo wakati akichangia majadiliano ya Taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utekelezaji wa mwongo wa Pili wa utokomezaji Umaskini mwaka – 2008-2017.

Katika taarifa hiyo ambayo imewasilishwa mbele ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya Uchumi na Fedha imebainishwa kuwa, licha ya kuwa Kidunia Idadi ya watu wanaoishi katika Umaskini imepungua, idadi ya watu Maskini Barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara imeongeza kufikia Watu Milioni 414 kwa takwimu za mwaka 2010.

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments are closed.