TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAWEKEZAJI NA MARAIS WA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAWEKEZAJI NA MARAIS WA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI

Like
334
0
Tuesday, 24 March 2015
Local News

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wawekezaji na Marais wa nchi 5 za Ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.

Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam, SAIDI MECK SADIKI  amesema kuwa,Marais hao PAUL KAGAME wa Rwanda, PIERRE NKURUNZINZA wa Burundi, YOWERI MUSEVENI wa Uganda, UHURU KENYATTA wa Kenya na JOSEPH KABILA wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na  jumla ya Wawekezaji 350.

Amesema Tanzania kwa mara nyingine imepata heshima ya kuandaa mkutano huo na kufafanua  kuwa, wawekezaji hao wamekwishaanza  kuwasili jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 22 , huku Marais wa nchi hizo wakitarajiwa kuwasili kuanzia Machi 24,2015.

Comments are closed.