TANZANIA: WITO WATOLEWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

TANZANIA: WITO WATOLEWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
262
0
Monday, 02 March 2015
Local News

WAKATI Tanzania inatarajia kuingia katika zoezi muhimu la Uchaguzi mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais Oktoba mwaka huu, Wito umetolewa kwa waandishi wa habari kutojihusisha na upande wowote wa Vyama vya Kisiasa na badala yake wafuate maadili ya kazi kwa maslahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha –ADC SAID MIRAJI wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa Uandishi wa Habari ni Taaluma inayopaswa kutumika bila kuegemea upande wowote.

Ameeleza kuwa endapo itatumika kwa ajili ya baadhi ya vyama vya Siasa italeta madhara makubwa ikiwemo upotevu wa amani iliyopo.

Comments are closed.