TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.
Hayo yamebainishwa Jana Jijini Dar es salaam na Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini–TCRA, Mhandisi James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasilino ulioandaliwa na shirika la kimataifa la mawasilino -ITU kwa kushirikiana na TCRA pamoja na benki kuu ya tanzania, ambao umeshirikisha washiriki 156 kutoka nchi mbalimbali duniani, lengo likiwa ni kuhakikisha huduma za fedha kupitia mitandao ya simu zinawafikia zaidi wananchi wanaoishi vijijini,
KILABA amesema huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini imepiga hatua kubwa ulimwenguni kwa kutoa fedha na kutuma kwa njia ya simu bila matatizo yoyote sanjari na kuwa na mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu.