TANZANIA YATOA WITO KWA WANANCHI WA BURUNDI KUMALIZA TOFAUTI ZAO

TANZANIA YATOA WITO KWA WANANCHI WA BURUNDI KUMALIZA TOFAUTI ZAO

Like
193
0
Friday, 29 May 2015
Local News

TANZANIA imetoa wito kwa wananchi wa Burundi kushirikiana kumaliza tofauti zao za kisiasa zinazoendelea nchini humo ili kurudisha hali ya Amani kwa manufaa yao naTaifa kwa ujumla.

 

Wito huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa BERNAD MEMBE wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum dokta MARY MWANJELWA alitaka kufahamu jitihada za serikali katika kusaidia Amani inarejea nchini Burundi.

 

Mheshimiwa MEMBE amesema kuwa ingawa kuna jitihada kubwa zinafanyika ili kurejesha Amani nchini Burundi lakini ni vyema wananchi husika wakajenga umoja ili kuleta maelewano baina yao.

Comments are closed.