TANZANIA YAUNGA MKONO MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO

TANZANIA YAUNGA MKONO MALENGO ENDELEVU YA MAENDELEO

Like
268
0
Monday, 28 September 2015
Local News

TANZANIA imeunga mkono Malengo Endelevu ya Maendeleo (Sustainable Development Goals – SDG’s), ikisisitiza kuwa malengo hayo ni silaha ya kutosha ya kufuta umasikini duniani katika sura zake zote ifikapo mwaka 2030.

Aidha imesema kuwa endapo dunia itafanikiwa kutekeleza malengo hayo ya SDG’s katika miaka 15 ijayo kama ilivyopangwa ni dhahiri kuwa ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa mahali pazuri zaidi.

Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalojadili kwa nia ya kupitisha SDG’s chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Lars Lokke Rusmussen.

Comments are closed.