TANZIA: Msanii Sam wa Ukweli Afariki Dunia

TANZIA: Msanii Sam wa Ukweli Afariki Dunia

1
1431
0
Thursday, 07 June 2018
Local News

MSANII wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu na mwili wake umehifadhiwa katika Hospital ya Mwananyamala.

 

Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake ambaye pia Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business aliyeeleza kwa masikitiko alivyopokea makubwa kuwa Sam amefariki dunia na kumtakia kupumzika kwa amani.

 

“Siamini kilichotokea muda huu ila sina jinsi, kwani woote safari ni moja, pumzika kwa amani Sam wa Ukweli, hakika nilikupenda kama ndugu yangu wakuzaliwa tumbo moja, #rip” amesema Amri the Business.

 

Aidha, aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Producer Steve amesema Sam alizidiwa zaidi Jumamosi iliyopita na walipomuuliza alisema ni ‘UKIMWI wa kulogwa’.

 

Sam wa Ukweli aliwahi kutamba na ngoma kama Sina Raha, Hata Kwetu Wapo, Sisikii, Milele na nyingine nyingi kali kuanzia mwaka 2010.

 

Uongozi wa Efm redio Unatoa pole kwa Ndugu jamaa na marafiki waliguswa na Msiba huu.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *