TARIME: JESHI LA POLISI LAPONGEZWA KWA KUIMALISHA ULINZI KIPINDI CHA UCHAGUZI

TARIME: JESHI LA POLISI LAPONGEZWA KWA KUIMALISHA ULINZI KIPINDI CHA UCHAGUZI

Like
351
0
Monday, 02 November 2015
Local News

KITUO cha sheria na haki za  binadamu wilayani Tarime Mkoani Mara kupitia mkurugenzi wake mtendaji Bonny Matto wamelipongeza Jeshi la polisi Kanda maalumu Tarime kwa kuimalisha ulinzi na usalama katika kipindi cha Uchaguzi.

 

Matto amesema kuwa kwa upande wa Tarime uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais umefanyika kwa amani na umekuwa  wa kihistoria kwani wananchi walijitokeza kwa wingi katika upigaji kura.

 

Amefafanua kuwa hayo yote ni matokeo ya juhudi za mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali na viongozi wa dini waliojitokeza kutoa elimu ya mpiga kura kwa watanzania.

Comments are closed.