TASAF YAPATIWA DOLA MILIONI 665 KUNUSURU KAYA MASIKINI

TASAF YAPATIWA DOLA MILIONI 665 KUNUSURU KAYA MASIKINI

Like
262
0
Friday, 18 March 2016
Local News

SERIKALI ya Tanzania imesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

 

Mkataba huo ambao umetiwa saini jijini Dar es Salaam unawataka watendaji kuweka utaratibu ambao unaenda sambamba na Mpango wa utekelezaji bila kuingilia majukumu ya mamlaka ya Serikali katika utekelezaji wa TASAF wa kunusuru kaya masikini.

 

Akizungumzia mkataba huo mara baada ya kusaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa mpango huo unaosimamiwa na TASAF unalenga kuziwezesha kaya masikini nchini kujiongezea kipato na kupata chakula cha kutosha pamoja na kujiletea maendeleo yao binafsi.

Comments are closed.