TCRA: SIMU BANDIA CHANZO CHA KUUNGUZA NYUMBA

TCRA: SIMU BANDIA CHANZO CHA KUUNGUZA NYUMBA

Like
295
0
Friday, 22 April 2016
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano Nchini-TCRA-imesema kuwa asilimia 79 ya simu za mkononi zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha mwezi disemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu sio bandia wakati asilimia 18 ya simu hizo ni bandia.

Aidha imeeleza kuwa asilimia kubwa ya nyumba zinazoungua kwa umeme kunatokana na simu bandia ambazo betri zake au vifaa vyake hushindwa kuhimili mionzi wakati zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha moto.

Hayo yamesemwa na meneja uhusiano wa mamlaka hiyo Innocent Mungi wakati akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za mkononi uliowashirikisha wadau na wafanyabiashara wa Jjini Arusha.

Comments are closed.