TCRA: SOFT BOX HAINA UWEZO WA KUFANYA UDUKUZI WA TAARIFA ZA MAWASILIANO

TCRA: SOFT BOX HAINA UWEZO WA KUFANYA UDUKUZI WA TAARIFA ZA MAWASILIANO

Like
251
0
Friday, 04 December 2015
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi na kubaini kuwa Application hiyo haina uwezo huo.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Application hiyo ya simu hivyo baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini na imejiridhisha kuwa program hiyo haina uwezo huo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi kama ilivyodaiwa. 

Comments are closed.