TCU YAFUTA VYUO VIKUU VISHIRIKI VIWILI

TCU YAFUTA VYUO VIKUU VISHIRIKI VIWILI

Like
325
0
Friday, 19 February 2016
Local News

TUME  ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU leo imevifuta  vyuo vikuu vishiriki viwili vya Sayansi za Kilimo na Teknolojia,  pamoja  na Teknolojia ya Habari   vya  Chuo cha Mtakatifu Yosefu Tanzania kutokana na kuwepo kwa matatizo ya muda mrefu ya ubora wa elimu, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu ambao hauzingatii matakwa ya Sheria ya Vyuo Vikuu.

 

Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa kifungu cha 5(1)cha Sheria ya Vyuo Vikuu , sura ya 346 ya Sheria za Tanzania  inasema Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.

Comments are closed.