TED CRUZ AJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO MAREKANI

TED CRUZ AJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO MAREKANI

Like
253
0
Wednesday, 04 May 2016
Local News

SENETA wa jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.

Cruz ametoa tangazo lake muda mfupi baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho Indiana.

Katika hatua nyingine Seneta wa Vermont- Bernie Sanders amemshinda Hillary Clinton kwenye uchaguzi wa mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Democratic katika jimbo la Indiana.

Comments are closed.