TED CRUZ AMBWAGA DONALD TRUMP KWENYE JIMBO LA UTAH

TED CRUZ AMBWAGA DONALD TRUMP KWENYE JIMBO LA UTAH

Like
291
0
Wednesday, 23 March 2016
Global News

LICHA ya kuongoza kwa mbali kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Republican, bilionea Donald Trump ameangushwa na hasimu wake Ted Cruz kwenye kura za mchujo za jimbo la Utah.

 

Wakati zaidi ya nusu ya kura zikiwa zimeshahesabiwa, Seneta Cruz anaongoza kwa takribani asilimia 70, huku Gavana John Kasich wa Ohio na Trump wakiwa nyuma yake.

 

Wiki iliyopita, Gavana Kasich alimshinda pia Trump kwenye uchaguzi wa Ohio.

Comments are closed.