TED CRUZ AMBWAGA TRUMP JIMBO LA WISCONSIN

TED CRUZ AMBWAGA TRUMP JIMBO LA WISCONSIN

Like
308
0
Wednesday, 06 April 2016
Global News

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa Donald Trump.

Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa.

Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa mgombea.

Comments are closed.