TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO YATAJWA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAPATO YA SERIKALI

TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO YATAJWA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAPATO YA SERIKALI

Like
192
0
Wednesday, 19 August 2015
Local News

MATUMIZI ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali imeelezwa kuwa yamepunguza upotevu wa mapato uliokuwa ukisababishwa na watendaji wasio waaminifu.

Kauli hiyo jijini Arusha  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Adorf Mapunda wakati akifunga awamu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa Serikali Mtandao uliowahusisha maafisa TEHAMA, Rasilimali watu, Utawala na Maafisa Habari kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema mabadiliko hayo ya ukusanyaji wa fedha kielektroniki yameongeza ufanisi kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuondoa wizi na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu.

 

Comments are closed.