TEMEKE: SEKTA YA UHANDISI IMETAKIWA KUANDAA MIRADI INAYOTEKELEZEKA

TEMEKE: SEKTA YA UHANDISI IMETAKIWA KUANDAA MIRADI INAYOTEKELEZEKA

Like
280
0
Monday, 25 January 2016
Local News

MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaurembo ameitaka sekta ya uhandisi pamoja na Watendaji wa Manispaa hiyo kuandaa miradi michache inayotekelezeka na kuwasilisha katika kamati ya maendeleo ya manispaa hiyo badala ya kuwa na miradi mingi isiyotekelezeka.
Chaurembo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kubaini kuwa miradi mingi haijakamilika kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ufinyu wa bajeti.
Aidha Chaurembo amewataka Wahandisi na Watendaji hao kuhakikisha wanasimamia uendelezaji wa manispaa hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema miradi mbali mbali ikiwemo ya ujenzi wa shule, barabara na zahanati.

Comments are closed.