TEMEKE WAANZA KUPATIWA HUDUMA YA AFYA KWA NJIA YA KADI

TEMEKE WAANZA KUPATIWA HUDUMA YA AFYA KWA NJIA YA KADI

Like
275
0
Friday, 04 December 2015
Local News

MFUKO wa afya ya jamii   umezindua rasmi huduma ya tiba (TIKA) kwa kadi katika Manispaa ya Temeke utakao mwezesha mwananchi  kupata hudua hiyo kwa gharama nafuu.

Akizungumza katika ufunguzi huo,  mkurugenzi wa mfuko  wa afya ja jamii – CHF, bwana Eugen Mikongoti amesema kuwa mpango huo ni mpango wa hiari ulioanzishwa kwa sheria namba 1 ya mwaka 2001  ambapo chini ya mpango huo mwana jamii anaweza kuchangia kiasi cha fedha kilicho kubalika katika mamlaka ya jamii ili kumwezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima .

Aidha amefafanua kuwa mwana chama wa TIKA atapata huduma zote za afya  ikiwemo huduma ya wagonjwa wa kutwa na kulazwa huduma za upasuaji kulingana na taratibu zilizo wekwa, Pamoja na huduma za rufaa pale zinapo hitajika.

Comments are closed.