TEMESA YATAKIWA KUWEKA WAZI HUDUMA ZAKE KWA JAMII

TEMESA YATAKIWA KUWEKA WAZI HUDUMA ZAKE KWA JAMII

Like
244
0
Monday, 20 April 2015
Local News

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mhandisi MUSSA IYOMBE,ameutaka Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini-TEMESA,kutangaza huduma wanazozitoa ili jamii inufaike na huduma hizo kwa wakati na gharama nafuu.

Akizungumza na Menejimenti ya TEMESA jijini Dar es salaam,Mhandisi IYOMBE, amesisitiza Wakala huo kuwa na Wafanyakazi wenye Weledi,waliokabidhiwa Mamlaka kamili na wabunifu ili kuhuisha huduma na kujiongezea mapato.

Pia ameagiza TEMESA kuimarisha uhusiano wake na jamii hasa sekta binafsi ili kubadili mtazamo uliopo sasa kuwa wakala huo unatengeneza magari ya Serikali peke yake,hivyo kushindwa kuteka soko la sekta binafsi.

 

Comments are closed.