TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

TETESI ZA MAGAZETI YA NG’AMBO

Like
371
0
Thursday, 22 January 2015
Slider

TETESI ZA MAGAZETI:

Klabu ya Manchester United imeweka mezani kitita cha paundi milioni 61 ili kumsajili kiungo wa klabu ya Juventus PAUL POGBA huku Chelsea nayo ikionekana kumuhitaji mchezaji huyo.

(Daily Express)

Klabu ya Valencia na Liverpool zimeingia katika kinyanganyiro  cha kuisaka saini ya kiungo wa Manchester City JAMES MILNER.

(Sky Sports)

Klabu ya Arsenal na Manchester United zipo katika kinyanganyiro cha kuisaka saini ya beki wa kati wa klabu ya Villarreal GABRIEL PAULISTA kwa paundi milioni 16.

(Daily Mail)

Klabu ya Chelsea ipo katika mazungumzo na klabu ya Fiorentina ili kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo JUAN CUADRADO kwa kitita cha paundi milioni 20.

(Guardian) 

Klabu ya Wigan Athletics imewekamezani paundi milioni 4 ili kumsajili mshambuliaji wa klabu ya West Brom  CALLUM McMANAMAN.

(Goal.com)

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea ANDRE SCHURRLE yupo tayari kuihama timu hiyo na kutimkia katika klabu ya nyumbani Wolfsburg.

(Independent)

 

Comments are closed.