TFDA YAKAMATA  DAWA NA VIPODOZI HARAMU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 135

TFDA YAKAMATA DAWA NA VIPODOZI HARAMU VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 135

Like
243
0
Monday, 14 September 2015
Local News

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA imefanikiwa kukamata dawa na vipodozi haramu vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 135, katika maeneo 243 kwenye Mikoa nane ya Tanzania Bara wakati wa Operesheni ya pili ya Giboia (Operesheni chatu) iliyofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Agosti Mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bwana Hiiti Sillo amesema baada ya uchambuzi na uchunguzi wa makosa kukamilika hatua mbalimbali zitachukuliwa pamoja na kuwapeleka Watuhumiwa mahakamani na kutoa adhabu kulingana na sheria ya chakula, Dawa na vipodozi sura 219 na sheria ya Famasia sura 311.

Comments are closed.