TFDA YATEKETEZA SHEHENA YA VYAKULA, VIPODOZI NA VIFAA TIBA KANDA YA KATI

TFDA YATEKETEZA SHEHENA YA VYAKULA, VIPODOZI NA VIFAA TIBA KANDA YA KATI

Like
332
0
Monday, 14 September 2015
Local News

MAMLAKA ya chakula na dawa –TFDA, kanda ya kati imeteketeza zaidi ya tani tatu za shehena ya vyakula, vipodozi vifaa tiba na dawa zenye thamani ya shilingi milioni 38. 8 kufuatia msako mkali uliofanywa katika maduka yaliyoko Manispaa ya Dodoma na kubaini bidhaa hizo hazifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kumalizika muda wa matumizi pamoja na kuwa na kemikali zenye viambata vya sumu.

Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Florent Kayombo amesema bidhaa hizo zimekamatwa kufuatia msako uliofanyika mwezi Jully na August ambapo pia jumla ya maduka tisa ya vipodozi yalifungiwa na kutozwa faini.

Comments are closed.