TGNP: VITUO VYA TAARIFA VIMESAIDIA KUFICHUA MAMBO YALIYOJIFICHA NA KUYAFANYIA KAZI

TGNP: VITUO VYA TAARIFA VIMESAIDIA KUFICHUA MAMBO YALIYOJIFICHA NA KUYAFANYIA KAZI

Like
285
0
Wednesday, 22 April 2015
Local News

MTANDAO wa jinsia Tanzania TGNP umesema kuwa kuwepo kwa vituo vya taarifa na Maarifa katika vijiji na sehemu mbalimbali nchini, kumeweza kusaidia kuleta mabadiliko kwa kufichua mambo  yaliyojificha na kuyafanyia kazi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mtandao wa TGNP LILIAN LIUNDI amesema kuwa, kama Serikali za Vijijini ,Kata na Mitaa vitaona umuhimu wa kutoa vipaumbele, vituo hivyo wataweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hasa wa Vijijini.

LIUNDI amewaomba Viongozi wa Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano kwenye vituo hivyo vya taarifa na maarifa,ili kusaidia kutatua kero wanazokabiliana nazo  ili kuendeleza  nchi ya Tanzania.

 

Comments are closed.