TGNP YAENDELEZA HARAKATI ZA KUDAI KATIBA MPYA YENYE KUZINGATIA MRENGO WA KIJINSIA

TGNP YAENDELEZA HARAKATI ZA KUDAI KATIBA MPYA YENYE KUZINGATIA MRENGO WA KIJINSIA

Like
309
0
Wednesday, 25 March 2015
Local News

MTANDAO wa Jinsia Tanzania-TGNP umesema kuwa, utaendeleza harakati za kuhakikisha kwamba, Wanawake wanatoa sauti ya pamoja katika kudai Katiba mpya inayozingatia mrengo wa Kijinsia.

Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa TGNP, LILIAN LIUNDI amesema , Wanawake wanatambua kuwa Katiba inayozingatia mrengo wa Kijinsia ni ile inayotokana na mchakato ulioshirikisha Sauti za Wanawake na Wanaume, na iliyoweka bayana makubaliano na Msingi Mkuu unaoongoza Tanzania.

Amesema kuwa kama Katiba itakua imejengewa msingi wa Usawa, Utu na Heshima ya Mwanamke na Mwanamme, ikiwa ni pamoja na kukataza aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji wa Kijinsia itaweza kumkomboa Mwanamke.

Comments are closed.