TGNP YAFANYA MAFUNZO KUELIMISHA WAZEE WA KIMILA

TGNP YAFANYA MAFUNZO KUELIMISHA WAZEE WA KIMILA

Like
237
0
Monday, 09 February 2015
Local News

MTANDAO wa kijinsia Tanzania TGNP umefanya mafunzo ya kuelimisha Wazee wa kimila katika Mikoa ya Mara, Shinyanga, Pwani, Dar es salaam, Mbeya na Morogoro lengo likiwa ni kuwapa Ujuzi wazee hao ili waweze kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

Akizungumza na EFM Afisa mawasiliano kutoka Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP MERKIZEDECK KAROLI amesema kuwa kupitia Semina hiyo itawawezesha wazee hao kujua endapo katika maeneo wanayoishi kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watu wanaofanya vitendo hivyo.

Aidha KAROLI amebainisha kuwa vita dhidi ya ukatili inahitaji nguvu ya pamoja kutoka kwa wananchi na viongozi ngazi zote katika kukomesha vitendo hivyo na sio kuwaachia mashirika ya kutetea haki za binadamu pekee.

Comments are closed.