TGNP YAFANYA TAMASHA LA KIJINSIA TARIME

TGNP YAFANYA TAMASHA LA KIJINSIA TARIME

Like
376
0
Monday, 02 March 2015
Local News

MTANDAO wa kijinsia Tanzania umefanya Tamasha la kijinsia ngazi ya Wilaya ya Tarime ikiwa na lengo la kutoa Elimu na uelewa kwa jamii juu ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mimba za utotoni, ukeketaji vipigo na umiliki wa Rasirimali.

Akizungumza na efm mtafiti shirikishi jamii kutoka TGNP AGNES LUKANGA amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mtandao wa TGNP hapa nchini mnamo mwaka 1993 TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ikiwa ni pamoja na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukeketaji.

Aidha amesema kuwa ukeketaji ni sawa na ukatili mwingine lakini pia ni kinyume cha haki za wanawake na watoto wa kike hivyo kuendeleza ukeketaji nchini Tanzania ni kwenda kinyume na mikataba ya kikanda na kimataifa ambayo Serikali imeridhia.

 

Comments are closed.