MTANDAO wa kijinsia Tanazania TGNP umelaani kitendo cha baadhi ya Wabunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushindwa kuhudhuria Vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini dodoma huku wakitumia kodi za wananchi waliowachagua bila manufaa yoyote na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Afisa mawasiliano kutoka TGNP MELCKDEZEL KAROLI amesema kuwa kitendo cha wabunge kutokuwepo ndani ya bunge wakati maamuzi mbalimbali yakiwa yanafanyika ni kuwanyima haki wananchi kwa kuwa wao ndio waliowachagua. Aidha amesema kuwa kwa sasa wabunge wengi wamekuwa wakikimbilia katika majimbo wanayoyaoongoza baada ya kushindwa kufanya kitu cha maana pindi walipochaguliwa hali inayopelekea kukimbilia katika majimbo yao ili waweze kuwaonyesha wananchi mambo ambayo watayafanya endapo watachaguliwa kwa mara nyingine. Hata hivyo amewataka wabunge kuelewa wajibu wao kwa wananchi waliowachagua na sio kukimbilia majimboni huku wakiacha vikao vya bunge vikiendelea ambako wananchi wanategemea uwakilishi wao.