TGNP YAWATAKA WANAWAKE KUACHA UTEGEMEZI

TGNP YAWATAKA WANAWAKE KUACHA UTEGEMEZI

Like
236
0
Tuesday, 21 April 2015
Local News

MTANDAO wa  Jinsia Tanzania –TGNP umewataka   Wanawake nchini kuacha tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wajishughulishe na kujikwamua kiuchumi ili  kuepukana na ukatili wa Kijinsia  unaowakabili  baadhi ya Wanawake wategemezi.

Hayo  yamesemwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa TGNP  DEO TEMBA, alipokuwa akizungumza na Kituo hiki juu ya  upingaji wa Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Amesema kuwa, katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huo, umebaini kuwa, kwa asilimi kubwa ukatili wa Kijinsia unawakabili Wanawake ambao hawajawezeshwa Kiuchumi hasa katika maeneo ya  pembezoni.

Comments are closed.