THAILAND YAANZA KUCHUNGUZA MAGAIDI

THAILAND YAANZA KUCHUNGUZA MAGAIDI

Like
228
0
Friday, 04 December 2015
Global News

POLISI nchini Thailand wanachunguza ripoti zinazoeleza kuwa wanamgambo kumi kutoka kundi la wapiganaji wa Islamic state wameingia nchini humo na wanapanga kushambulia sehemu zinazomilikiwa na Urusi.

Taarifa hizo zimeeleza kwamba Sita kati yao wameripotiwa kuelekea maeneo ya kifahari ya Pattaya na Phuket huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Hata hivyo Polisi nchini humo wamesema kuwa hawajafanikiwa kuthibitisha uwepo wa raia hao wa Syria nchini Thailand.

Comments are closed.