Aliyekuwa kinara kwenye mchezo wa gofu duniani Tiger Woods ameporomoka katika viwango vya dunia vya mchezo wa gofu baada ya kutolewa katika orodha ya mia bora.
Eldrick Tont Woods ambae ni raia wa Marekani hii ni mara kwanza kushuka kiwango katika historia yake ya kipindi cha uchezaji wa mchezo huo.
Woods ambaye ni bingwa mara 14 aliingia mia bora kwa mara ya kwanza mwaka 1996 ameweka rekodi ya kuwa bingwa wa dunia kwa wiki 683, lakini sasa ameteremka mpaka nafasi ya 104.
Kwa sasa mchezaji huyu ameonyesha kutokatishwa tamaa na matokeo hayo na kuelezea matumaini yake ya kurejea katika kiwango chake katika shindano kubwa la mwaka la Masters litakaloanza April 9 mwaka huu.