TISHIO LA BOMU LAILAZIMU NDEGE YA EGYPT KUTUA GHAFLA

TISHIO LA BOMU LAILAZIMU NDEGE YA EGYPT KUTUA GHAFLA

Like
283
0
Wednesday, 08 June 2016
Local News

NDEGE ya shirika la EgyptAir ambayo ililazimika kutua nchini Uzbekistan kutokana na udanganyifu wa kuwepo kwa bomu, imeruhusiwa kuendelea na safari yake kutoka Cairo kwenda Beijing.

 

Abiria wote 118 na wafanyikazi 17 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, waliondolewa katika uwanja wa kimataifa wa Urgench.

 

Wiki tatu zilizopita ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka mjini Paris kwenda Cairo ikiwa na abiria 66 ilianguka katika bahari ya Mediterranean.

Comments are closed.