TMA: MVUA ZA MASIKA ZITAKUWA ZA WASTANI

TMA: MVUA ZA MASIKA ZITAKUWA ZA WASTANI

Like
419
0
Friday, 04 March 2016
Local News

UTABIRI wa Hali ya Hewa kwa mvua za masika zinazoanza wiki hii nchini umeonesha kuwa zitakuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya nchi huku baadhi ya maeneo zikiwa chini ya wastani.

 

Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi mkuu wa malaka ya Hali ya Hewa Tanzania dokta Agnes Kijazi ambapo amesema katika maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria, Nyanda za juu, Kaskazini Mashariki pamoja na maeneo machache ya mkoa wa Tanga mvua zitanyesha hadi juu ya kiwango.

 

Mvua za masika katika kipindi cha mwezi machi hadi Mei mwaka huu zinatarajiwa kuanza wiki hii katika mikoa ya Kagera na Mara na kusambaa katika mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu.

Comments are closed.