TMA YAANZISHA MFUMO UTAKAOWEZESHA MARUBANI KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA MTANDAO

TMA YAANZISHA MFUMO UTAKAOWEZESHA MARUBANI KUPATA TAARIFA KWA NJIA YA MTANDAO

Like
222
0
Monday, 23 March 2015
Local News

KATIKA kuadhimisha siku ya hali ya hewa duniani, Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA imeanzisha mfumo ambao utawawezesha marubani wote kupata taarifa mbalimbali za safari za anga kwa njia ya mtandao ambapo kila shirika la ndege limepewa namba ya siri  ya kuingia kwenye mfumo huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Masoko na Mahusiano kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa HELLEN MSEMO amesema kuwa kwa kufanya hivyo mamlaka imeweza kutekeleza mpango ujulikanao kama Quality Management System unaosaidia kutoa huduma za usafiri wa anga ambazo zitawafikia walengwa kwa wakati.

Kila ifikapo Machi 23 ya kila mwaka Shirika la hali ya hewa duniani huadhimisha siku ya hali ya hewa ikiwa na kauli mbiu ya mwaka huu inasema, Uwelewa wa hali ya hewa kwa maamuzi stahiki.

Comments are closed.