TMA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI USHIRIKISHAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

TMA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI USHIRIKISHAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Like
307
0
Thursday, 04 June 2015
Local News

KATIKA kudhibiti athari za majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mafuriko, mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA-imekutana na wadau mbalimbali kujadili juu ya ushirikishaji wa taarifa za hali ya hewa ili kupunguza madhara hayo.

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wadau hao leo jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa –TMA– dokta LADISLAUS CHANG’A amesema kuwa ili kudhibiti majanga hayo ni muhimu kwa kila mtu kuwa mfuatiliaji wa masuala ya hali ya hewa kila inapotolewa na mamlaka hiyo.

CHANG’A amesema kuwa katika kuhakikisha suala hilo linamfikia kila mmojawapo kwa usahihi mamlaka inashirikiana na ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza hali ambayo inasaidia kupatina kwa takwimu na kuimarisha ushirikiano wao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma mheshimiwa RAMADHAN MANENO amesema kuwa masuala ya hali ya hewa ni muhimu katika nchi yoyote katika kujiimarisha hivyo ni vyema yakazingatiwa ipasavyo.

Hata hivyo MANENO ameiomba serikali kuchukua jitihada za dhati katika kuhakikisha inaboresha huduma za utoaji taarifa za mamlaka hiyo kwa wananchi ili kuwasaidia kujiepusha na madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa.

Comments are closed.