TMA YATAKA MAANDALIZI KUFUATIA HOFU YA MVUA ZA ELNINO

TMA YATAKA MAANDALIZI KUFUATIA HOFU YA MVUA ZA ELNINO

Like
264
0
Thursday, 03 September 2015
Local News

KUFATIA uwepo wa viashiria vya kunyesha mvua nyingi zinazosababishwa na Elnino ambazo mara nyingi husababisha mafuriko,  Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA- wamezitaka mamlaka za serikali  na taasisi binafsi kuandaa mapema  mazingira yatakayosaidia kuepukana na athari za mafuriko hayo.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Dokta Agnesi Kijazi amesema ni vyema kwa sekta ya uchukuzi ambayo mara nyingi huathirika zaidi pindi mafuriko yanapotokea kuandaa mazingira ya kukabiliana na uharibifu wa miundombinu.

 

Dokta Kijazi ameitaka menejimenti ya maafa kuandaa mazingira mapema ikiwa ni pamoja na kutenga fungu la kukabiliana na hali ya mafuriko yanayotarajiwa kuwa kama yale ya mwaka 1997 au zaidi huku akiwataka wananchi waishio mabondeni kuhama maeneo hayo ili kuepusha maafa makubwa kutokea.

Comments are closed.