TMA YATOA TAARIFA YA MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA

TMA YATOA TAARIFA YA MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA

Like
344
0
Tuesday, 03 March 2015
Local News

MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini-TMA  imetoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa kipindi cha Mwezi Machi hadi Mwezi Mei mwaka huu ambapo inaonesha kuwa maeneo mengi ya nchi hayatakuwa na kiwango cha mvua cha kuridhisha.

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dokta AGNES KIJAZI amesema kuwa ingawa hali ya mvua haitarajiwi kuwa ya kuridhisha lakini kuna baadhi ya maeneo yanatarajiwa kupata Mvua za wastani hadi juu ya wastani ikiwemo Kanda ya Ziwa Viktoria na maeneo ya Kusini mwa nchi.

Dokta KIJAZI amesema kuwa katika maeneo ambayo yanapata mvua mara mbili kwa mwaka lakini si za kuridhisha ni muhimu kwa wananchi katika maeneo husika kuzitumia mvua hizo kwa manufaa zaidi.

Comments are closed.