WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uingereza,TONY BLAIR ameingia katika kampeni za uchaguzi kwa kumshambulia Waziri Mkuu DAVID CAMERON, kwa ahadi yake ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu uanachama wa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, EU.
Bwana BLAIR amesema Bwana CAMERON ametoka nje ya agenda kwa kuahidi kufanyika kura ya maoni na kwamba kujiondoa katika Umoja wa Ulaya kunatishia nafasi ya Uingereza kama taifa kubwa duniani
Bwana BLAIR anatarajiwa kusema kuwa kiongozi wa Chama chake cha LABOUR ED MILIBAND ameonyesha ukomavu kiuongozi kwa kuhimili shinikizo la wanaotaka kura ya maoni kuhusu Uingereza kuendelea kuwa Mwanachama wa EU au kujitoa.