TRA KUKUSANYA KODI KUFIKIA MALENGO YA KUIWEZESHA SERIKALI

TRA KUKUSANYA KODI KUFIKIA MALENGO YA KUIWEZESHA SERIKALI

Like
437
0
Monday, 13 July 2015
Local News

MAMLAKA ya mapato Tanzania –TRA– imedhamiria kufikia malengo yake katika ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kufikia shilingi trilioni 22.3 iliyojiwekea katika bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016.

 

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  Rished Bade wakati wa Semina ya wahasibu iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi –NBAA– kwa lengo la kujadili kuhusu masuala ya kodi, bajeti na uchumi kwa ujumla.

 

Naye Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Nicholus Duhia ameahidi kuwa bodi yake itashiriki vyema katika kuhakikisha inaleta mabadiliko chanya katika sekta ya Kodi nchini.

TRA2 TRA4

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.

Comments are closed.