TRA YAANDAA SEMINA NA WADAU WA MICHEZO

TRA YAANDAA SEMINA NA WADAU WA MICHEZO

Like
197
0
Friday, 14 August 2015
Local News

KUFUATIA Serikali kupitisha sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya Mwaka 2014 iliyoanza kutumika rasmi Julai Mosi Mwaka huu, Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA imeandaa semina na wadau mbalimbali wa Michezo kujadili utekelezaji wa kodi hiyo katika sekta ya michezo kwa kuwa Sekta hiyo inamchango mkubwa wa mapato ya Serikali endapo itatumika vizuri.

Semina hiyo ya siku moja imewashirikisha TFF na Wadau mbalimbali wa Michezo kwa lengo la kutoa mafunzo maalum juu ya sheria mpya ya kodi ya ongezeko la thamani -VAT ili kuingiza rasmi sekta hiyo katika mfumo wa ukasanyaji mapato.

Comments are closed.