TRA YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KATIKA KIPINDI CHA MWEZI DESEMBA 2015

TRA YAKUSANYA TRILIONI 1.4 KATIKA KIPINDI CHA MWEZI DESEMBA 2015

Like
254
0
Wednesday, 06 January 2016
Local News

JUMLA ya shilingi trilioni 1.4 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

 

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi  bilioni 490 kwa mwezi ikilinganishwa na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

 

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

Comments are closed.