TRA YAWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA BIASHARA ZA MAGENDO

TRA YAWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA BIASHARA ZA MAGENDO

Like
280
0
Monday, 02 February 2015
Local News

MAMLAKA ya mapato Tanzania –TRA, imewataka wananchi kujiepusha na biashara za magendo kwani adhabu zinazotolewa kwa wahusika wanaokamatwa na na biashara hizo ni kali na zinarudisha nyuma maendeleo yao Taifa.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano wa TRA Richard Kayombo na kuongeza kuwa ni wakati sasa wananchi wanapaswa kuinua uchumi wa nchi yao kwa kulipa kodi.

Kayombo ameongeza kuwa TRA imejipanga kikamilifu kwani kipo kikosi kinachoitwa fast Team ambacho kipo mahususi kwa ajili ya kupambana na njia zote za panya zinazoingiza bidhaa kwa kukwepa kulipa kodi,hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kikosi hicho ili kuwezesha zoezi hilo kwa maendeleo ya nchi .

Aidha ameongeza kuwa `hatua zinazochukuliwa na TRA hivi sasa wanapokamata bidhaa hizo za magendo wanataifisha na mali zote za kila atakaekamtwa nazo lengo likiwa ni kuondoa mianya ya yoye magendo.

Comments are closed.