TRENI MBILI ZAKOSEA NJIA NA KUTUMBUKIA MTONI INDIA

TRENI MBILI ZAKOSEA NJIA NA KUTUMBUKIA MTONI INDIA

Like
201
0
Wednesday, 05 August 2015
Global News

TRENI mbili zimekosea njia huko nchini India na kutumbukia katika mto uliokuwa umefurika kufuatia mvua kubwa katika Jimbo la Madhya Pradesh.

Shirika la habari la Associated Press limemnunukuu mmoja wa waokoaji akisema kuwa wamehesabu maiti 20 na  kwamba zaidi ya abiria 250 wameokolewa, baada ya mabehewa sita kutumbukia katika mto huo.

Wakuu wa shirika la Reli la India wanasema ajali hiyo ilitokea usiku wa manane kuamkia leo jumatano.

 

Comments are closed.